Thursday , 25th Jul , 2024

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata Musa Sasi (32) mkazi wa Goba Matosa baada ya kumuua mpenzi wake Lucy Stevin Haule (29) mfanyakazi wa kiwanda cha pombe kali iitwayo nguvu banana wine huku chanzo cha ugomvi huo zikiendelea kuchunguzwa.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum SACP Jumanne Muliro

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum SACP Jumanne Muliro, na kusema taarifa za mauaji hayo wamezipata asubuhi ya leo Julai 25, 2024, ambapo Musa baada ya kumuua mpenzi wake naye alijaribu kujiua kwa kutumia kisu, kwa kujichoma shingoni.

"Mtuhumiwa huyo amekamatwa na hali yake ni mbaya na yupo Hospitali ya rufaa ya Mwananyamala, chanzo halisi cha ugomvi ulipolekea mauji hayo bado kinachunguzwa," amesema SACP Muliro

Aidha Kamanda Muliro ameongeza kuwa, "Jeshi la Polisi linatoa wito pindi watu wanapokuwa na migogoro au matatizo ya kijamii wazishirikishe taasisi mbalimbali za kisheria, za kiserikali na zisizo za kiserikali lakini pia taasisi za kidini ili zisaidie kutatua matatizo ya wahusika,".