Wakizungumzia tukio hilo baba na mama wa watoto hao wamesema kuwa wakati tukio hilo linatokea jana majira ya saa moja jioni, mama alikuwa dukani akihudumia mteja aliyempigia simu kwa ajili ya kuuziwa kuni.
Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Kagera linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini chanzo cha moto huo na kutoa tahadhari kwa wazazi kuwalinda watoto wao.
Watoto waliofariki kwa moto ni Justa John (9) alikuwa Mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya Mubembe na Julietha John (4) #EastAfricaTV