Tuesday , 23rd Jul , 2024

 Waziri wa Maji Jumaa Aweso, amemsimamisha kazi, Meneja wa usambazaji maji Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) Eng Thomas Ngulika kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Meneja aliyesimamishwa

Waziri Aweso ametangaza uamuazi huo leo Jumanne tarehe 23 Julai 2024 akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Morogoro.

"Hatutokuwa tayari kuona mtu kwa maksudi anatoa taarifa za uongo, wakati yeye ndiye anayehusika katika hilo jambo, eneo la Tungi, nane nane na maeneo mengine wiki tatu hawakupata maji, namuuliza Mtendaji anaongea uongo wewe unamwambia moja mbili tatu karekebishe, anarekebisha leo watu wanapata maji" amesema Waziri Aweso na kuongeza

"Huyu mtu wetu ambaye anahusika na suala la Technical atatupisha, bodi ipo hapa mumsimamishe mara moja la pili acha mimi niende kwenye kikao ipo timu yangu hapa inanifanyia kazi nitawasaidia lakini lazima twende" ameeleza.