Akizungumzia kuhusu kuelekea uzinduzi wa shindano hilo,Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ) Kanali Martin Msumari amesema matayarisho yote yamekamilika huku akitoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kushuhudia michuano hiyo ambayo haina kiingilio.
“lengo la mashindano hayo yenye kauli mbiu 'Ushindi ni Heshima', ni kuimarisha afya, umoja na mshikamano wa majeshi” Kanali Msumari
Kwa upande mwingine,Mkufunzi wa mpira wa mikono kutoka timu ya Ngome Shafizi Issa amesema wamejiandaa kutetea ubingwa wao hivyo wanatuma salamu kwa kamandi zote wajiandae kupata kichapo kutoka kwao kwenye shindano hilo