Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam,Rais wa CECAFA Wallace Karia amesema mashindano hayo yamekuwa na mvuto kutokana na upinzani uliopo na kuahidi kuzidi kuyaboresha zaidi kwenye msimu unaofuata wa mwaka 2025
"Mashindano haya yanazisaidia timu kufanya maandalizi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya msimu ujao pamoja na yale ya Kimataifa nina ahidi kuyaboresha zaidi hapo mwakani, amesema Karia.
Hatua ya nusu fainali ya michezo ya CECAFA 2024 inataraji kuchezwa kesho Jijini Dar es Salaam ambapo mchezo wa mapema timu ya APR ya Rwanda itapambana na Al Hilal Omdurman FC ya Sudan Saa 9 Alasiri kwenye dimba la KMC Complex-Mwenge huku Al Wadi FC ya Sudani itapambana na Red Arrows ya Zambia Saa 1 Usiku kwenye dimba la Azam Complex Chamazi –Mbande