(Mchezaji Mpya wa Yanga SC Prince Dube)
Dube amesema “Nafurahi kucheza Yanga,kuna wachezaji wakubwa hapa na kila mchezaji anatamani kucheza ndani ya Yanga ni timu kubwa na nipo hapa kwa ajili ya kufanya kazi nimepitia kipindi kigumu na sasa natamani kufurahi na kuitumika klabu kwa sasa”
Kwa upande mwingine,Dube amezungumzia kuhusu mbio za ufungaji bora ndani ya msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara 2024-25 na kusema kwa sasa mawazo yake yapo kuisaidia klabu hiyo kubeba mataji na kushinda mechi pekee.
“kuhusu kiatu cha ufungaji bora hiyo ni kazi nyingine,mimi nipo hapa kuisadia klabu kushinda michezo na mataji lakini kama mshambuliaji unamuomba Mungu akusaidie sasa ikitokea nitamuomba Mungu lakini jambo la kwanza kusaidia timu kushinda mechi na makombe na kuongeza thamani yangu binafsi”- amesema Prince Dube
Prince Dube amejiunga na Yanga SC ndani ya msimu huu kama mchezaji huru baada ya kumalizana na klabu yake ya zamani ya Azam FC aliyojiunga nayo mwaka 2020 akitokea klabu ya Highlanders ya nchini Zimbabwe