Wednesday , 17th Jul , 2024

Mmiliki wa mtandao wa ''X'' Bilionea Elon Musk kupitia mtandao huo ametangaza rasmi dhamira yake ya kuhamisha makao makuu ya mtandao wa ''X'' pamoja kampuni ya ''Space X'' kutoka San Francisco, California kuhamishia Austin, Texas. 

 

Ikumbukwe huku Austin, Texas ndipo pia yalipo makao makuu ya kampuni yake ambayo inajihusisha na uzalishaji wa magari inayofahamika kama Tesla, 

Sababu kadhaa zinatajwa kufikia uamuzi huo wa ndugu Elon Musk
1. Wingi wa magenge ya uhalifu yaliyopo California ambayo ameyataja kama usumbufu kwenye kampuni yake.

2. Mabadiliko na upitishwaji wa muswada unaofahamika kama AB 1955. Muswada ambao unazuia wazazi kutokupata taarifa pale ambapo mtoto wao atabadilisha jina au jinsia yake kwenye taarifa za shule, 

Awali wakati muswada huu unatambulishwa lengo kubwa lilikuwa ni kuwaweka wazi wazazi kuhusiana na mabadiliko yoyote ya mtoto ikiwa kama amebadili jina au jinsia lazima mzazi apewe taarifa.

Lakini muswada mpya uliotiwa saini na Gavana - Gavin Newsom wa jimbo la California unawataka walimu kudanganya wazazi ikiwa kama mtoto amebadili jina au jinsia kwenye taarifa za shule (kuto kusema ukweli)

Sababu kubwa aliyokuja nayo Elon Baada ya haya yote ni kudai kwamba kupitishwa kwa sheria hii itakuwa kama shambulio kwa familia nyingi zinazoishi kwenye jimbo hilo, na kuongeza kuwa mwaka mmoja nyuma alikwishafanya mazungumzo na Gavana Gavin Newsom kumueleza kwamba iwapo atapitisha mswada huo atasababisha familia na kampuni nyingi kulihama jimbo hilo ili kuwalinda watoto wao dhidi ya muswada huo.