(Aliyekuwa Mkufunzi wa England Gareth Southgate)
Southgate mwenye umri wa miaka 53 amesema "Najivunia kuwa Muingereza,ni heshima kubwa kwenye maisha yangu kuichezea England na kuifundisha England lakini kwa sasa ni muda wa mabadiliko na ukurasa mpya ndani ya timu”
Gareth Southgate amedumu ndani ya England kwa miaka 8 huku ameiongoza kwenye michezo 102,kushinda michezo 64,Sare michezo 20 na kupoteza kwenye michezo 18 huku akiwa na asilimia ya ushindi 65.2% huku anakumbukwa kuifikisha England hatua ya Nusu Fainali ya kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.
Mkataba wa Gareth Southgate ulikuwa unamalizika Desemba 2024 huku tayari majina ya makocha kama Mauricio Pochettino,Graham Potter,Eddie Howe yanatajwa kwenda kurithi mikoba ya Southgate ndani ya England.