MOdester Malahya, Mkazi wa Halawa
Kaimu meneja wa RUWASA wilaya ya Bariadi mhandisi Herry Magoti amesema bajeti iliyopangwa kwaajili ya utekelezaji wa mradi huo kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ni kiasi cha shilingi milioni 49 huku mkuu wa wilaya ya Bariadi Simon Simalenga akisema lazima mradi huo utekelezwe kwa manufaa ya wananchi wote.
“Katika mwaka wa fedha huu tuliokamilisha 2023/24 kijiji cha Halawa tulitenga fedha takribani milioni 49 kwaajili ya kuboresha kisima kirefu ambacho kina pump ya mkono ile pump ya mkono tunaitoa tunafunga pump ya umeme inamaana umeme wa jua yaani solar na tunaweka simtank la lita 5000 na tunasambaza mtandao wa maji km 2.1 tulitangaza tender hiyo mkandarasi akapatikana serikali ya kijiji pamoja na mkutano mkuu wa kijiji wa wananchi walitusitisha kwamba kile kisima tusikitumie waendelee kutumia pump ya mkono”Hery Magoti, Kaimu meneja wa RUWASA Bariadi.
“Nyie mnaosema maji yasiende kule ni kina nani leo mkandarasi yupo site muda mrefu na vifaa vimefika hapa mradi hautekelezwi maana yake ni nini” Simon Simalenga, Mkuu wa wilaya ya Bariadi.