Thursday , 27th Jun , 2024

Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi linafanya uchunguzi wa tukio la kuokotwa kwa kijana Edger Mwakalebela maarufu kama Sativa, mkazi wa Dar es Salaam, mfanyabiashara aliyekutwa na majeraha kichwani katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani,

Taarifa hiyo imetolewa leo Juni 27, 2024, na Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani, ambapo taarifa yake imeeleza namna Sativa alivyokutwa, "Baada ya kuokotwa alieleza kuwa alitekwa toka tarehe 23.6.2024 akitokea kwa rafiki yake akielekea nyumbani kwake Mbezi kwa Msuguri ndipo alitekwa na watu ambao hakuweza kuwatambua na kumpeleka hadi jijini Arusha na baadae mkoani Katavi na kutelekezwa katika pori la hifadhi ya Taifa ya Katavi,".

Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa, "Hivi sasa anaendelea na matibabu wakati uchunguzi wa tukio hili ukiendelea kwa kushirikiana na taasisi nyingine za kichunguzi,".