Monday , 24th Jun , 2024

Mbunge wa Geita vijijini Joseph Kasheku Msukuma, ameomba mwongozo kwa Naibu Spika wa Bunge kuhusu sakata la wafanyabiashara wa Kariakoo kufunga maduka yao hii leo Juni 24, 2024.

Kulia ni maduka ya Kariakoo yaliyofungwa

Akizungumza bungeni hii leo mbunge Msukuma amesema kuwa, "Mhe Naibu Spika naomba kuanza kuomba mwongozo wangu kwa kutumia lugha ya Dar es Salaam, wanasema kazini kwako kuna kazi, kumekuwa na kipeperushi kinatembea mitandaoni kuhusiana na wafanyabiashara wa Kariakooo na sehemu zingine kufunga maduka leo, na tunapozungumza sasa hivi Kariakoo imefungwa hakufanyiki biashara lakini pia sisi wabunge kuna mambo tuliyataja kwenye michango yetu,".

Aidha Mbunge Msukuma ameongeza kuwa, "Natambua kwamba kamati ya wafanyabiashara iko hapa kwa ajili ya kuzungumza na serikali, watu wetu wa vijijini wameenda Dar es Salaam kufuata mahitaji wamekuta Kariakoo imefungwa na wengine hawana nauli wanaanza tena kuomba kwetu wabunge. Nini kauli ya serikali kuhusu wafanyabiashara waliofunga maduka leo,"

Akijibu hoja hiyo Naibu Spika wa Bunge amejibu, "Toka jana na leo serikali na viongozi wa wafanyabiashara wanakutana na taarifa rasmi tutaipata baada ya kikao hicho kumalizika,"