Nyumba iliyoteketea kwa moto
Wakizungumza kwa huzuni wazazi wa watoto hao wamesema walikuwa hawajarudi nyumbani wakati moto unaanza kuwaka, na wakati wanarudi walishtushwa kuona moto mkubwa unawaka na kuteketeza nyumba na mali zote, na kupelekea vifo vya watoto hao.
Kwa upande wa majiarani na mashuhuda wa tukio hilo wamesema wakati wanafika moto ulikuwa unawaka kwa kasi kubwa na kufanikiwa kumuokoa mtoto mmoja, huku wakishindwa kuingia ndani kumuokoa mtoto mwingine aliyekuwemo.
Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Mwanza Kamila Labani, anasema pamoja na jitihada za uokozi walizofanya lakini tayari mtoto mmoja amefariki huku mwingine akifariki akiwa hospitali na chanzo cha moto ni mtoto mmojawapo kuwasha moto kwenye godoro.