Wednesday , 12th Jun , 2024

Mahakama ya Wilaya ya Gairo imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Michael Mchanjale (31) baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumbaka na kumpa ujauzito mtoto wa dada wa mke wake mwenye umri wa miaka 14.

Gerezani

Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Irene Lyatuu amesema kuwa mahakama imempa adhabu hiyo baada ya kuzingatia ushahidi wa pande zote mbili.

Mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Septemba 22, 2023 majira ya saa tatu usiku ambapo mtoto huyo alikwenda nyumbani kwa mshtakiwa kwa lengo la kujihifadhi mara baada ya kupigwa na kufukuzwa na mama yake wa kambo anayeishi naye.

Katika hukumu ya shauri hilo, upande wa Jamhuri uliowakilishwa na wakili wa serikali, Elias Masini umeiomba mahakama itoe adhabu inayostahili ili iwe fundisho kwa watu wengine kutokana na kitendo hicho kwani hukwamisha ndoto za mabinti wengi .

Mahakama imesema rufaa ya hukumu hiyo iko wazi kwa upande wowote ambao haujaridhika na uamuzi uliotolewa ndani ya muda wa kipindi cha siku 30.