Thursday , 30th May , 2024

Kwenye miaka ya 1980, kipindi ambacho Michael Jackson yuko kwenye ubora wa muziki wake, alichukua sura tofauti kwenye macho ya watu kwa uamuzi wake wa kuishi na sokwe ambaye alipewa jina la Bubbles.

Bubbles, ni aina ya sokwe ambaye kupatikana kwake njia za maabara ilihusika na kukua kwake ilibidi apelekwe kwa mtaalamu wa wanyama Bob Dunn ili kufunzwa na kupatiwa matibabu.

Bubbles, aliyeonekana kula maisha na kutembea nchi mbali mbali ambazo Michael alienda kwa lengo la kutoa burudani, alijizolea umaarufu mkubwa kwenye kona mbali mbali za dunia.

Lakini maswali ya watu wengi ni kwamba sokwe yule yuko wapi kwa sasa?

Ni miaka 15 hivi sasa tangu umauti ulipo mkuta Michael, lakini taarifa nzuri ni kwamba Bubbles, bado yuko hai na kwa sasa anamiaka 40 kwa mujibu ''unilad.com'' na anaishi kwenye kituo cha kulelea sokwe huko Florida nchini Marekani na huduma zake za kumtunza ni zaidi ya Milioni 64 kwa mwaka.

Picha:  Getty Images