![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2024/03/25/mgaya.jpg?itok=F7MGSBSu×tamp=1711399727)
Dkt. Prosper Mgaya, Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji nchini (NIT)
Akizungumza na wadau wa usafirishaji kutoka Mikoa ya Mwanza, Geita na Mara, Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji nchini (NIT) Dkt. Prosper Mgaya amesema katika kuhakikisha usalama unaimarika chuo hicho kinakutanisha wadau wa usafirishaji ili kuweka mikakati ikayosaidia kumaliza tatizo hilo.
Aidha, Dkt. Mgaya amebainisha kuwa ipo haja ya kutafuta mwarobaini wa ajali hizo ambazo zinapunguza nguvu kazi ya taifa.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ilemela Hassan Masala amekitaka chuo hicho kuendelea kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa sheria za usalama barabarani ili kusaidia kupunguza ajali za barabarani.