Monday , 11th Mar , 2024

Shughuli za usafirishaji zimekwama hii leo jijini Mwanza kwa baadhi ya wananchi kutokana na mgomo wa daladala ulioanza asubuhi ya leo.

Wakazi wa Mwanza wakitembea kwa mguu baada ya daladala kugoma

EastAfricaTV imepita katika mitaa mbalimbali jijini humo kushuhudia nauli zikipanda kwa usafiri wa bodaboda na bajaji, huku sababu kubwa ya mgomo ikitajwa kuwa ni muingiliano katika kazi baina ya bajaji na daladala.