Wa kwanza kukutana na Simba kwenye dimba hilo watakuwa ni Wajelajela Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu utakaochezwa Machi 6, mwaka huu.
Kwa sasa uwanja huo unaendelea kufanyiwa maboresho hasa katika eneo la kuchezea (pitch) na imeamuliwa kwamba usitumike kwa shughuli nyingine zaidi ya soka.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima amesema lengo la mkoa, chama cha soka na wamiliki wa uwanja huo ni kufanya maboresho zaidi ili uwe na hadhi ya kutumiwa na timu zitakazoshiriki #AFCON2027 kwa ajili ya mazoezi.