
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Kamishina wa kanda Maalum CP Muliro Jumanne Muliro amesema tukio hilo lilitokea Februari 18 Mwaka huu majira ya Saa tatu usiku wakati mtu huyo aliyejifanya Mganga wa wajadi na kuingia nyumbani kwa familia ya Mzee Halisi Amani kwa lengo la kumtibia mke wake Fatuma Abdallah (52) aliyekuwa anasumbuliwa na tatizo la miguu.
“Aliwanywesha Dawa iliyowalewesha familia nzima wakapoteza fahamu na kuwaibia simu tano za mkononi na kuondoka" amesema Kamishina Muliro
Kamishina Muliro ameongeza kuwa kufuatia tukio hilo jeshi limetoa onyo kwa wanaojifanya waganga wakienyeji kuwa halitosita kuwachukulia hatua.
Katika hatua Nyingine Jeshi hilo limewataka Mamlaka husika inayohusika Sukari kuuza kwa bei elekezi na hatosita kuwachukulia hatua