
Taarifa iliyotolewa na msemaji wa familia ya Mzee Mwinyi, Abdullah Ali Mwinyi inaeleza kuwa kutokana na ushauri wa madaktari wake, familia imeona ni vyema apate faragha akiwa anapatiwa matibabu, hivyo Familia inaiomba jamii kumkumbuka kwenye Dua, Sala na Maombi.
"Tunamuomba Mwenyezi Mungu amjaalie shifaa ya haraka Mzee wetu pamoja na wagonjwa wengine wote wanaokabiliwa na maradhi mbali mbali" Abdullah Ali Mwinyi Msemaji wa Familia