Friday , 2nd Feb , 2024

Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Bazn Berhe kutokea Virginia nchini Marekani, amejikuta akidondokea kwenye hukumu nzito ya kifungo cha miaka 100 baada ya kukutwa na kosa la mauaji.

Bazn Berhe (25) inatajwa alihusika kwenye mauaji ya mfanyakazi mwenzake baada ya kumshtumu kuwa alimuibia chakula chake alichohifadhi kwenye jokofu la kazini kwao

Kulingana na waendesha mashtaka, Wanadai kuwa Berhe alikasirika baada ya kugundua kwamba Leiva ambaye alikuwa mfanyakazi mwenzake, amechukua chakula chake cha mchana kutoka kwenye jokofu la ofisi.

Ndipo Bazn Berhe aliamua kununua visu viwili siku mbili kabla ya kutekeleza mauaji, na siku iliyofuata aliitumia kupata mafunzo ya mauaji, waendesha mashtaka walisema wakati wa kusikilizwa kwa hukumu ya Berhe alitishia kuua watu wengine ikiwa hatapewa hukumu kali zaidi.

Picha: kiro7.com