Kocha aliyejiunga na Liverpool mwaka 2015 akaomba muda kwa ajili ya kuanza kuvikusanya vikombe kuanzia 2019 kuendelea akatimiza ahadi zake kwa vitendo.
Rasmi leo hii kupitia ukurasa wa timu hiyo amefunguka kwa kusema mwishoni mwa-msimu huu ataagana rasmi na timu hiyo, ni ngumu yeye kuiyeleza na ngumu pia watu kuipokea.
Hadi sasa haijafahamika rasmi ni kwa nini uamuzi wa namna hiyo umekuwa wa haraka zaidi kwa kocha huyo, Lakini baadhi ya makocha wanatajwa kuchukua nafasi yake ni pamoja na Xabi Alonso na Jose Mourinho.