Tuesday , 3rd Mar , 2015

Taasisi ya Tanzania Women of Achievement imetangaza leo wadhamini wakuu wa tuzo zinazosubiriwa kwa hamu mwaka huu za Tanzania Women of Achievement Awards (TWAA) ambayo inatarajia kufanyika Machi 7, 2015.

Rais wa Tanzania Women of Achievement Bi. Irene Kiwia said, “Tunayofuraha kubwa sana kutangaza kwenu washiriki hawa waliojumuika nasi katika kudhamini hii tukio la kipekee ambayo inalenga kusherehekea mafanikio ya wanawake na jinsi ambavyo wameweza kunufaisha jamii inayowazunguka.

Aliwataja wadhamini hao wakuu kama hoteli ya Dar es Salaam Serena, Delloite, TCRA, Multi-choice, National Reinsurance Corporation (TAN-RE), EATV and Radio, Frontline Porter Novelli, Thinline consultancy, East Coast Africa Music (ECAM), TSN, GRM Production na Print Galore.

“Tuzo za Tanzania Women of Achievement Awards sasa zinaenda mwaka wake wanne na zimeweza kuwa mfano tosha wa kuwapatia fursa wanawake kwa kutambua na kuwapongeza kwa kazi zao nzuri wanazoendelea kufanya katika kuifanya Tanzania kuwa sehemu nzuri zaidi.

“Tunataka kuwatambua wale wanawake ambao wameleta tofauti ya ukweli katika nyanja mbali mbali muhimu nchini Tanzania. Kwahiyo vigezo vya kushinda ni itakuwa safari yake ya maisha na namna ambavyo alivyoweza kupita katika kipindi kigumu, jinsi anavyowatia moyo wengine kama mfano mzuri wa kuigwa, kuleta mabadiliko katika jamii zao, umuhimu wao katika jamii na jinsi walivyoweza kugusa taifa kwa ujumla.”

Tuzo za mwaka huu zitatolewa kutokana na eneo la kundi na fani mbali mbali kama Sanaa na Utamaduni, Ujasiriliamali wa Kibiashara, TEHAMA, Michezo, Ya kiweledi kazini, Elimu, Afya, Ustawi wa Jamii, Sayansi na Teknolojia, Sekta ya Umma, Tuzo ya mafanikio kama Kijana, Kilimo, Mafanikio ya Kimaisha pamoja na tuzo kuu la Mwanamke Bora wa mwaka.

Majina ya washiriki wote yalipendekezwa kutoka kwa watu binafsi au mashirika kupitia www.twa.or.tz, au [email protected] na sasa tunamalizia kupiga mahesabu ya kura. Leo hii tunawatangazia majina matatu matatu kwa kila kundi la tuzo kabla ya kufanyika kwa tuzo hizo katika siku ya wanawake duniani.

Mwenyekiti wa TWAA Bi. Sadaka Gandi alisema, “Wakati uwezeshaji wa wanawake imekuwa ikipewa kipaumbele duniani kote, tuzo hizi zinalenga kutambua kazi za wanawake kwa ubunifu wao na miradi yao mbali mbali kutoka kwao wanawake katika namna tofauti. Tunaamini kwa washindi hawa watakuwa mfano kwa kila mtu kuanzia wasichana wadogo walio vijijini Tanzania mpaka wafanyabiashara wanawake na watunga sera nchini na zaidi.”

“Kwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo tumekuwa tukiwasihi kupendekeza majina ya wanawake wa kipekee ambao wanastahili kutambuliwa, kutoka mjasiriliamali wa kibiashara au mwalimu mzuri hadi mtu ambaye amebadilisha jamii yake na kuwa bora zaidi. Na sasa tumeshapokea mapendekezo yote hayo,” alisema Bi. Gandi.

Majina ya washiriki wote yalipendekezwa kutoka kwa watu binafsi au mashirika kupitia www.twa.or.tz, au [email protected] na sasa tunamalizia kupiga mahesabu ya kura. Leo hii tunawatangazia majina matatu matatu kwa kila kundi la tuzo kabla ya kufanyika kwa tuzo hizo katika siku ya wanawake duniani.

KAMATI YA MAJAJI
Kamati ya majaji wa TWAA inajumuisha Bi. Mary Rusimbi – Mwanaharakati na muasisi wa Tanzania Gender Networking Program (TGNP), Jaji Joaquine De Mello, Dk. Marcelina Chijoriga – Dean wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam idara ya Biashara, Innocent Mungy‐ Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Tanzania Communication Regulatory Authority (TCRA), Sadaka Gandi – Mshauri nasaha na mfanyakazi wa kijamii, Irene Kiwia – Muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Frontline Porter Novelli.

Wadhamini wa zamani
Wadhamini wa zamani ni Baileys, Delloite, NBC, Home Shopping Center, TCRA, Songas, The American People, DTP, UN Development Partners Gender Group, UNFPA, UNESCO, UN Women, TBL, Multichoice, Africa Life Assurance, Barrick, Twiga Cement, Vodacom, Farm Equip Company RBP, Clouds FM, Thinline, Costech, Kairuki Hospital, ZARA Tours, Serena Hotel, Tigo, African Lynx Investment, EATV na EA radio na Frontline Porter Novelli.

KUHUSU TAASISI YA TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA)

TWA ni taasisi isiyo ya kiserikali, ya hiari na kujitegemea inayojihusisha na uwezeshaji wa wanawake iliyoanzishwa mwaka 2009. Lengo kuu la TWA ni kuimarisha ushiriki, na majukumu ya wanawake na uwezo wao katika jamii ya Tanzania kwenye mambo ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni.

TWA inafanya kampeni, mafunzo, semina, mikutano na warsha ambazo zinakuza ubadilishanaji wa taarifa na ushauri kwa wanawake na wasichana wadogo wa Kitanzania. Kampeni na mafunzo haya yanalenga zaidi haki za binadamu na za wanawake, usawa wa kijinsia, na ushiriki wa wanawake kwenye shughuli za kiuchumi na kijamii.

Kazi kubwa ya TWA ni kuboresha maisha, kupanua fursa, na kuwasaidia wanawake Tanzania kushamiri na kuchangia kwenye ustawi wa nchi. TWA inafanya kazi na viongozi, watu binafsi, jamii, mashirika yasiyo ya kiserekali, serikali, sekta binafsi na wafadhili wa nje kujenga ufanisi na kuhakikisha malengo ya kuendeleza wanawake yanafanikiwa. TWA imejikita kwenye maendeleo ya Tanzania kuhakikisha kila mwanamke anakuwa chachu ya maendeleo.