Ahmed Ally amesema hayo wakati akizungumzia maandalizi ya kikosi cha Simba kuelekea michezo yao miwili inayofuata, mchezo wa kesho wa Ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar na wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca utakaochezwa Disemba 19.
“Kufika robo fainali tutafanikisha kwa kila Mwanasimba kuhusika kwa kuja uwanjani. Malengo yetu ni nusu fainali na itakuwa aibu kubwa sana tusipofika robo fainali. Na Simba ya sasa nyie wenyewe mnaiona, timu ina mabadiliko makubwa.” Amesema Ahmed Ally
Kwa upande mwingine Ahmed amethibitisha kuwa waamuzi watakao chezesha mchezo wao dhidi ya Wydad Casablanca wanatoka nchini Gabon, Cameroon na Kenya. Lakini bado wapinzani wao Wydad hawajathibitisha watakuja nchini lini kwa ajaili ya mchezo huo.