Tuesday , 5th Dec , 2023

Watu 14 wamefariki dunia nchini Thailand baada ya basi la abiria kupinduka barabarani na kugonga  kwenye mti.

Picha mtandaoni zinaonyesha basi hilo likiegemea upande wake na sehemu zake za mbele zikigawanyika nusu, huku sehemu za mti zikiwa zimeloa ndani yake.

Watu wengine 32 wamejeruhiwa kufuatia ajali hiyo iliyotokea katika eneo la Prachuap Khiri Khan, mkoa wa pwani kusini mwa nchi hiyo.Thailand ina moja ya viwango vya juu vya ajali za barabarani duniani, na kusababisha maelfu ya vifo kila mwaka.

Wengi wanataja hii kwa viwango duni vya usalama kwenye barabara zenye shughuli nyingi nchini humo.

Mwaka 2022 pekee, watu 15,000 walipoteza maisha yao katika barabara za Thailand, kwa mujibu wa Kituo cha Takwimu za Ajali za Barabara nchini humo. Nchini Uingereza, ambayo ina idadi ndogo ya watu, idadi hiyo ni 1,700.

Mnamo mwaka 2021, matukio yanayohusiana na trafiki yalijumuisha karibu theluthi moja ya vifo vyote nchini, Shirika la Afya Duniani lilisema