Monday , 2nd Mar , 2015

Askofu wa kanisa katoliki jimbo kuu la Moshi Mhashamu Issack Amani amewataka Watanzania waliozaliwa wakiwa na viungo timilifu kuwahurumia na kuwasaidia watu wenye ulemavu kwa hali na mali.

Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dr. Regnaldi Mengi.

Aidha wanatakiwa kutambua kuwa ugumu wa maisha wanauona wao kwa watu wenye ulemavu ni mara dufu na hawakuomba kuzaliwa na ulemavu

Askofu amani ameyasema hayo katika harambee ya ujenzi wa shule ya watoto wenye ulemavu inayojengwa na kanisa hilo katika kijiji cha Kimashuku kata ya Machame Kusini Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dr. Regnaldi Mengi aliyekuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo iliyowezesha kupatikana kwa zaidi ya milioni 400 yeye mwenyewe akiahidi kusaidia milioni mia mbili kila mwaka kwa kipindi cha miaka mitano amesema kila aliyezaliwa mzima ajue kuwa analo deni mbele ya mungu la kuwasaidia wenzao wenye waliozaliwa na ulemavu.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki katika harambee hiyo wamesema moyo wa kujitolea kuwasaidia watu wenye ulemavu na makundi mengine wakiwemo maskini unaoonyeshwa na Dr.regnald mengi unahitaji kuigwa na kuendelezwa na jamii yote na ni jambo linalowezekana .

Harambee hiyo iliyoshikisha makundi mbali mbali ya watu wakiwemo wafanyabiashara wakubwa ,viongozi wa dini wadau wa elimu ana wananchi wa kawaida ilitarajiwa kukusanya zaidi ya milioni mia nane ambapo shule inayojengwa inatarajiwa kugharimu zaidi ya bilioni sita.