Wednesday , 22nd Nov , 2023

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila, amefungua soko la Mbagala Zakhem lenye thamani ya shilingi bilioni 2.48 huku akiwataka watendaji kuhakikisha wanasimamia mapato kwa ufanisi jambo ambalo litasaidia kuleta tija kwa kuendelea kufanya maboresho katika maeneo ya kufanyia biashara

Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika hafla ya ufunguzi wa soko hilo RC Chalamila amesema kuwa mtendaji yeyote atakayebainika analeta ubabaishaji atamchukulia hatua za kisheria, huku akiwataka wafanyabiashara wote kuanza kufanya biashara ndani ya mwezi mmoja katika soko hilo.

Meneja wa Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) wilaya ya Temeke Mhandisi Paul Mhere, amesema kuwa lengo la mradi ni kuboresha miundombinu ya soko, kuongeza mapato na idadi ya wafanyabiashara kutoka 208 hadi 500.