Mvua
Mvua hizo zinatarajiwa kunyesha katika Mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, Lindi, Mtwara, Tanga na visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba.
Kupitia taarifa ya Mamlaka iliyotolewa jana Jumanne Novemba 21, 2023, imetaja athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na baadhi ya barabara kutopitika kutokana na mafuriko pamoja na vifo kwa siku hizo, hivyo wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari.