Wednesday , 8th Nov , 2023

EATV & EA RADIO Kwa kushirikiana na TASACI tumekabidhi ped kwa wanafunzi wa shule ya msingi Mabwepande kwa lengo la kuhakikisha watoto wetu wanapata hedhi salama.

 

EATV & EA Radio kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TASACi) wamekabidhi pedi kwa wanafunzi wa kike wa Shule ya Msingi Mabwepande, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuhakikisha watoto wa kike wanapata hedhi salama na yenye heshima.

Zoezi hilo limefanyika katika shule hiyo iliyopo Mabwepande, jijini Dar es Salaam, likiwa na lengo la kupunguza changamoto zinazowakabili wanafunzi wa kike wakati wa hedhi, ikiwemo utoro shuleni, aibu na kukosa vifaa sahihi vya kujisitiri.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, mwakilishi wa EATV & EA Radio alisema kuwa taasisi hiyo inaendelea kutumia jukwaa lake kuhamasisha masuala ya kijamii yanayogusa maisha ya watoto, hususan wasichana, huku akisisitiza kuwa hedhi siyo aibu bali ni sehemu ya kawaida ya ukuaji wa mtoto wa kike.

Kwa upande wake, mwakilishi wa TASACi alieleza kuwa mamlaka hiyo itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha elimu ya hedhi salama inawafikia watoto mashuleni pamoja na jamii kwa ujumla, ili kujenga kizazi chenye uelewa na afya bora.

Walimu na uongozi wa Shule ya Msingi Mabwepande wameishukuru EATV & EA Radio pamoja na TASACi kwa msaada vhuo, wakieleza kuwa utawasaidia wanafunzi wa kike kuendelea na masomo yao bila vikwazo vinavyotokana na changamoto za hedhi.

Zoezi hili ni sehemu ya kampeni endelevu ya kuhamasisha hedhi salama na kulinda haki ya mtoto wa kike kupata elimu bila kikwazo chochote.