Monday , 23rd Oct , 2023

Rapa wa Marekani Blueface amejitokeza hadharani kumsema mama yake mzazi kwamba alikuwa 'Kahaba' kwa sababu ameolewa mara 3 na kupata watoto watatu kwa wanaume watatu tofauti.

Picha ya rapa Blueface

Blueface amefunguka hilo kupitia mtandao wake wa 'X' akieleza kuwa mama yake alipenda sana pesa hivyo alikuwa ana-force kudai talaka kwa wanaume alioolewa nao ili kugawana maokoto.

Ameongeza kusema hiyo ni story ya kusikitisha kutoka kwa mama yake na hakuweza kumuheshimu tena kama mwanamke.