Friday , 20th Oct , 2023

Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Patrice Motsepe amelitambulisha rasmi kombe ambalo atakabidhiwa bingwa wa michuano ya African Football League (AFL)

Motsepe ametambulisha kombe hilo jijini Dar es salaam amesema Msimu ujao watakuwa  na timu 24 kwenye michuano ya African Football League nawatazipata  kupitia ranki za CAF pamoja na mafanikio  katika ligi za nyumbani.

"Nawashukuru viongozi wa timu zote nane zinazoshiriki michuano ya African Football League pamoja na zile 24 ambazo zitashiriki mwakani." Rais wa CAF, Patrice Motsepe.

Wakati huo huo Rais Motsepe amekutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Samia Suluhu Hassan katika ikulu chamwimo Mkoani Dodoma