Thursday , 19th Oct , 2023

Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amefanya mazungumzo na viongozi wa Israel mjini Tel Aviv na anatarajiwa kuzuru nchi nyingine katika eneo hilo.

 

Alipowasili, alilaani  kitendo cha kutisha cha ugaidi  kilichofanywa  na Hamas mnamo 7 Oktoba, na kusema Uingereza inasimama na Israeli.

Jeshi la Israel linasema lilishambulia mamia ya maeneo ya Gaza katika kipindi cha saa 24 zilizopita, likilenga  miundombinu ya Hamas.

Gaza bado inazingirwa, huku Israel ikizuia usambazaji wa maji, umeme na mafuta.

Lakini Marekani na Misri zinasema malori yanayotoa misaada yanapaswa kuanza kuvuka kutoka Misri kuingia Gaza siku ya Ijumaa.

Joe Biden amerejea Marekani - ziara yake fupi nchini Israel iligubikwa na mlipuko katika hospitali moja ya Gaza, ambayo maafisa wa eneo hilo wanasema iliwaua watu 471, idadi inayopingwa na Israel.

Mamlaka za Palestina zinasema shambulio la anga la Israel lilikuwa la kulaumiwa - lakini Israel inasisitiza kuwa mlipuko huo ulisababishwa na roketi iliyorushwa kutoka Gaza

Wafanyakazi wa misaada wanasema wamekuwa wakisubiri upande wa Misri wa kuvuka Rafah kwa siku kadhaa sasa wakati wakisubiri ruhusa ya kuruhusiwa kuingia na kusambaza vifaa vya dharura