Wednesday , 18th Oct , 2023

Rais wa Marekani Joe Biden amewasili Israel kukutana na waziri mkuu Benjamin Netanyahu.

Ameahidi msaada wa Marekani na kusema shambulio la hospitali ya jana usiku huko Gaza "limeonekana" kuwa limesababishwa na "timu nyingine"

Israel inasema mlipuko huo uliotokea Jumanne jioni ulisababishwa na roketi iliyorushwa vibaya na wanamgambo wa Kipalestina.

IDF inasema ushahidi wake unaonyesha roketi ya Islamic Jihad ya Palestina, iliyofyatuliwa kutoka makaburini, ilitua katika eneo la kuegesha magari ya hospitali.

Hamas, mamlaka za Palestina na nchi nyingine zinailaumu Israel kwa mlipuko huo, ambao Hamas inasema uliuwa watu 500.

Israel imefanya mashambulizi ya anga katika maeneo yote ya Gaza tangu mashambulizi ya Hamas Oktoba 7

IDF inasema takriban roketi 450 zilizofyatuliwa kutoka Gaza tangu wakati huo zimetua katika ardhi ya Gaza.

K wa upande wake Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amrsema "ulimwengu uliostaarabika lazima uungane ili kuishinda Hamas" kwa njia ile ile iliyofanya wakati wa kuchukua IS.

Anasema lengo ni kuishinda Hamas na kuondoa kitisho hiki cha kutisha kutoka sio tu kwenye maisha ya Wa Israel bali ni ya kila mtu.

Anamwita Biden kuwa "rafiki wa kweli" na anapongeza uamuzi wake wa "kusonga sana" kutembelea Israeli wakati wa vita.