Monday , 16th Oct , 2023

Unaweza kusema like Father like Son mtoto wa Rapa Drake aitwaye Adonis ameachia Freestyle ya "My Man" ambayo imewavutia wengi baada ya mtoto huyo kuonesha uwezo wa kutembea na mistari kwenye beat ya Hip Hop licha ya kuwa na umri mdogo wa miaka 6.

Picha ya Drake na mtoto wake Adonis Graham

Hii inaonesha kuwa mtoto huyo amerithi kile anachofanya mara zote baba yake na Drake ameshare kipande cha ngoma hiyo na kumtakia heri ya kuzaliwa mtoto wake kupitia mtandao wake wa Instagram na kuwapa taarifa mashabiki zake kuwa "My Man Freestyle" imetoka.