Friday , 6th Oct , 2023

Maboresho ya Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Jijini Dar es Salaam yamezidi kushika kasi huku wadau wanaoutumia uwanja huo wataanza kupata huduma ya bure ya mtandao (internet) pindi wakiingia ndani ya uwanja huo.

baadhi ya maeneo yamefanyiwa marekebisho makubwa kuelekea mchezo wa ufunguzi wa Africa Super League baina ya Simba dhidi ya Al Ahly ya Misri huku sasa mashabiki watafurahia huduma ya bure ya mtandao pindi waiingiapo uwanjani hapo.

Kwa upande mwingine,Mahona amezidi kuwa sisitiza mashabaki na wadau wote wanaoutumia uwanja huo kuendelea kuwa wastaarabu kwa kutunza miundombinu ya uwanja kwa kuwa unatumia fedha nyingi kwa ajili ya marekebisho na matengenezo.

Uwanja wa Benjamin Mkapa ulianza kutumika rasmi mnamo mwaka 2007 huku sasa upo kwenye mchakato wa marekebisho makubwa yanayogharimu kiasi cha Bilioni 31 na unatarajia kukamilika mnamo Juni 2024.