Friday , 6th Oct , 2023

Michuano mikubwa ya ligi ya mpira wa kikapu ya NBL (National Basketball League) inayotarajiwa kuanza Jumamosi ya Oktoba 7, 2023 Jijini Dodoma na kutamatika Septemba 13, 2023 kwa kushirikisha Mabingwa wote wa Mikoa yenye ligi za mpira wa kikapu.

Mashindano hayo pia yatakuwa na ongezeko la timu nane kwa upande wa wanawake na wanaume zilizotinga hatua ya nusu fainali mwaka 2022 ambazo ni Pazi ambao ndio mabingwa watetezi wa nchi, ABC, Kisasa na Wakuda wakati kwa timu za wanawake ni VBQ ambao ndio abingwa watetezi wa nchi, Jkt Stars, Db Pantellin na Bandari Queens.