Tuesday , 26th Sep , 2023

Rais Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga, kwamba ashughulikie uboreshaji wa mitambo ya umeme na baada ya hapo hataki kusikia kelele za umeme kukatika hovyo.

Rais Samia Suluhu Hassan

Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 26, 2023, jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni.

Rais Samia amesema kwamba, changamoto ya umeme iliyopo hivi sasa ni kutokana na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa ikiwemo jua kali hali inayopelekea ukame kwenye vyanzo vya maji, hivyo anaamini uboreshaji wa mitambo utakapokamilika Tanzania itaondokana na tatizo la umeme kukatika.

"Mkurugenzi mpya wa TANESCO nenda kaanzie pale maharage alipofikia, najua utaweza nakupa miezi sita nakuangalia pale, kazi yako ya kwanza ni kusimamia ukarabati wa mitambo ya umeme, lakini baada ya miezi sita nisisikie kelele tena za kukatika kwa umeme," amesema Rais Samia.