Sunday , 24th Sep , 2023

Mwanariadha Mtanzania Magdalena Shauri amevunja rekodi ya Taifa ya marathon kwa wanawake baada ya kukamata nafasi ya tatu kwenye mashindano ya Berlin Marathon kwa kilometa 42 akitumia saa 2:18:41.

Mashindano hayo yametimua vumbi leo Septemba 24, 2023 nchini Ujerumani huku Magdalena akitanguliwa na Tigist Assefa kutoka Ethiopia aliyemaliza wa kwanza kwa saa 2:11:53 na Mkenya Sheila Chepkirui aliyemaliza nafasi ya pili akitumia saa 2:17:49.

Magdalena ambaye alikuwa akichuana na wakimbiaji mashuhuri duniani kutoka Ethiopia, Kenya, Marekani, Uganda, Uingereza na nchi nyingi duniani akimaliza nafasi ya tatu na kujikatia tiketi ya kushiriki michuano ya Olympic itakayofanyika Paris nchini Ufaransa mwakani.