Thursday , 21st Sep , 2023

India imesitisha huduma za viza kwa raia wa Canada huku kukiwa na mzozo mkubwa kuhusu mauaji ya Sikh wanaotaka kujitenga katika ardhi ya Canada.

 

Mtoa huduma za visa BLS alituma ujumbe kutoka kwa ujumbe wa India akilaumu "sababu za kiutendaji" kwa uamuzi huo. Mvutano ulizuka wiki hii baada ya Canada kusema inachunguza "madai ya kuaminika" yanayoihusisha India na mauaji ya kiongozi huyo wa wanaotaka kujitenga.

India ilikataa kwa hasira madai hayo na kuyaita "ya kusikitisha". Wachambuzi wanasema uhusiano kati ya nchi hizo ambazo zimezorota kwa miezi kadhaa, sasa uko katika kiwango cha chini kabisa.

Ujumbe kuhusu kusimamishwa kwa visa ulichapishwa kwa mara ya kwanza kwenye tovuti ya BLS siku ya Alhamisi.

Wizara ya mambo ya nje ya India ilikataa kuzungumzia suala hilo na kuitaka BBC kurejelea tovuti ya BLS.

Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya India kutoa ushauri wa kuwataka raia wake wanaosafiri kwenda au wanaoishi Canada "kuchukua tahadhari kubwa" kwa kuzingatia "kuongezeka kwa vitendo vya chuki dhidi ya India na uhalifu wa chuki na uhalifu wa jinai nchini Canada".