
Idadi hiyo inaweza kuongezeka maradufu, waziri wa utawala wa mashariki anaongeza.Mafuriko yaliharibu mabwawa mawili katika mji wa pwani ya mashariki na kusomba nyumba.Barabara zimefunikwa na matope na vifusi na zimejaa magari yaliyogeuzwa.
Libya imegawanyika kati ya serikali mbili hasimu, huku moja ikiendeshwa kutoka Tripoli na nyingine upande wa mashariki.
Mabwawa mawili yalibomoka katika bonde la Derna wakati wa dhoruba kubwa, na kusababisha maji mengi kukimbia kuelekea baharini na kuharibu mji wa pwani.
Mtaalamu mmoja ameiambia Al-Wasat, tovuti ya habari inayoongoza nchini Libya, kwamba mabwawa hayo hayakutunzwa vizuri.
Maelfu bado hawajulikani waliko, na waziri kutoka utawala wa mashariki alisema: "Bahari inatupa miili kadhaa kila wakati".
Takriban watu 34,000 wamelazimika kuyahama makazi yao katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko, na picha zinaonyesha matukio mabaya, huku milima ya vifusi, magari yaliyovunjwa na mifuko ya mwili ikiwa imetanda mitaani.