
Rais Volodymyr Zelensky ameliambia shirika la habari la Interfax-Ukraine kwamba Ukraine haikuhusika katika kifo cha bosi wa Wagner Yevgeny Prigozhin
Ndege hiyo inayomilikiwa na Prigozhin, ilikuwa na abiria saba na wafanyakazi watatu wakati ilipoanguka katika eneo la Tver. Miili yote 10 imepatikana, ripoti zinasema
Kufuatia ajali hiyo na vifo hivyo kumekua na mshangao baada ya Rais wa Urusi Vladimir Putin wa Urusi kutotaja ajali hiyo wakati akihutubia mkutano wa kimataifa kwa njia ya video.
Hata ikulu ya Kremlin bado haijasema lolote kuhusu ajali ya ndege ya Jumatano ambapo kiongozi wa Wagner Yevgeny Prigozhin anadhaniwa kuwa amefariki dunia.
Kuna uvumi mkubwa juu ya kile kilichotokea. Vyanzo vya ulinzi vya Uingereza vinaiambia BBC kuwa shirika la ujasusi la Urusi FSB lina uwezekano mkubwa wa kuwajibika.
Wakati huo huo , Rais Volodymyr Zelensky ameliambia shirika la habari la Interfax-Ukraine kwamba
Ukraine haikuhusika katika kifo cha bosi wa Wagner Yevgeny Prigozhin. Rais huyo amesema nchi yake haijahusika na suala hilo na kwamba anatambua ni nani ana uhusiano na suala hilo