Saturday , 19th Aug , 2023

Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Mbeya (CCM) Bahati Keneth Ndingo amejiuzulu nafasi hiyo ili agombea ubunge wa Jimbo la Mbarali katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni

Bahati amejuzulu nafasi hiyo kwa mujibu wa lbara ya 149 (1) (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. 

Katika barua yake kwa Spika, ameeleza sababu za kujiuzulu ni kuangalia namna nyingine ya kuwatumikia Watanzania katika Bunge.

"Ninakusudia kushiriki kwenye mchakato wa Uchaguzi Mdogo wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Mbarali unaotarajiwa kufanyika siku za hivi karibuni" imeeleza barua hiyo.