Wednesday , 9th Aug , 2023

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini DCI Ramadhani Kingai, amewataka Maofisa, Wakaguzi na Askari wa Jeshi la Polisi kufanya upelelezi kabla ya kumkamata mtuhumiwa.

DCI Ramadhan Kingai (Katikati), wakati akizungumza na Maafisa wa Jeshi la Polisi

Hayo ameyasema leo Agosti 9, 2023 alipofanya kikao kazi na Askari wa vyeo mbalimbali wa Mkoa wa Kipolisi Rufiji.

Amewataka Maofisa, Wakaguzi na Askari wawafikishie elimu hiyo wananchi ili watambue kwamba upelelezi unatakiwa ufanyike kabla ya mtuhumiwa kukamatwa.

Na kwamba pindi mtuhumiwa anapopatikana au kukamatwa wapelelezi waandae jalada ili lipelekwe katika Ofisi ya  Mkurugenzi wa Mashtaka kwa ajili ya kuandaa hati ya mashtaka ili mtuhumiwa afikishwe mahakamani.