Monday , 7th Aug , 2023

Kituo cha Utafiti cha Jeshi la Polisi kilichopo Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam kwa kushirikina na TICD, imeendelea na mafunzo kwa kundi la wanafunzi wa kozi ya uofisa ambayo yamelenga kuwajengea uwezo na maarifa mapya katika kupambana na ukatili wa kijinsia.

Mhadhiri Msadizi kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Elinami Nassari, akitoa mafunzo kwa Maofisa

Mkuu wa kitengo cha utatifi cha Jeshi la Polisi ndani ya chuo hicho Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Ralph Meela, amesema kuwa kazi kubwa ya kituo hicho ni kufanya tafiti na kushirikiana na Taasisi za Elimu ya Juu katika kuwaongezea uwezo Maafisa na Askari wa Jeshi hilo.

Ameongeza kuwa tayari zaidi ya taasisi 10 zimeshafika chuoni hapo kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa maafisa wanafunzi na Wakaguzi Wasaidizi wa Polisi huku akimshuru Mkuu wa Jeshi hilo IGP Camillus Wambura, kwa namna ambavyo amewaunganisha na taasisi za elimu ya juu katika kufanya maboresha ya utendaji kazi unaoendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

Kwa upande wake Mhadhiri Msadizi kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Elinami Nassari, amebainisha kuwa ni muhimu Jeshi la Polisi kushirikisha jamii na kuzielewa kwa kina jamii ambazo wanakwenda kuzihudumia ambapo amewaomba maafisa hao wanafunzi kufahamu mila na tamaduni husika ili kutengeneza ushirikishwaji wa jamii kikamilifu na wenye matokeo chanya.