Saturday , 29th Jul , 2023

 Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile amesema, safari ya mabadiliko ya sheria ya habari haijafika mwisho

Akizungumza katika siku ya pili ya semina kwa wahariri iliyohusu mapitio ya Sheria ya Huduma ya Habari (MSA) iliyopitishwa na bunge hivi karibuni amesema, bado kuna shida katika sheria hiyo na kwamba, kwenye maboresho ya kanuni zake mambo mengi yatabadilika.

“Hatujafika mwisho wa uhuru wa habari. Bado tunaendelea na vitu vingine vitabadilishwa kupitia kanuni za sheria ya habari. Tuendelee kushirikiana na taasisi zote kwani bado kuna matatizo kwenye sheria hii" 

“Tunakwenda kuzungumza na serikali kuhusu leseni za magazeti ambapo tutashauri iwe kwa miaka 15, hakuna sababu ya kusajili leseni ya magazeti kila mwaka,” amesema na kuongeza

“Mara nyingi tunazungumzia magazeti lakini kuna tatizo kwenye socila media, Televisheni pamoja na Radio, hawa wanapata tabu kupitia TCRA (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania). tunataka sheria zote zisimamiwe sehemu moja,” amesema Balile