Mtoto anayenyanyaswa na aliyekaa chini ni Anastazia Jackson
Wananchi hao wameeleza kuwa tangu watoto hao watatu wafiwe na mama yao mzazi dada yao huyo ambaye ni wa kambo amekuwa akiwatesa watoto hao ikiwemo kuwanyima chakula pamoja na kuwatumikisha kazi ngumu.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Iborero Stephano Samson pamoja na Kamanda wa Sungusungu wamefika katika familia hiyo na kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha polisi huku baba mzazi wa mtoto huyo akitoroka eneo la tukio.
Wanaume waliofika katika tukio hilo wamelaani vitendo vya ukatili vinavyofanywa na watu wanaokabidhiwa kuwalea watoto baada ya wazazi kufariki dunia huku wakiviomba vyombo vya dola kuchukua hatua kali ili iwe fundisho.