Saturday , 8th Jul , 2023

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema tarari Viongozi wa Mkoa wa Dar es salaam wameanza kufanyia kazi sakata la clip inayosambaa inayohusu Mtumishi wa Afya akichambua, kusafisha na kuanika vifaa vya Hospitali katika Hospitali ya Kivule Mkoani Dar es Salaam.

Waziri Ummy amesema Kitendo hicho ni kinyume na taratibu na miongozo ya Kanuni za Udhibiti wa Maambukizi (Infection Prevention and Control). 

"Tayari Viongozi wa Mkoa wa Dar es salaam wanalifanyia kazi suala hili na watatoa Taarifa Rasmi" 

Aidha Waziri Ummy amemshukuru mwananchi alierekodi na kuisambaza clip hii na kuwataka wananchi kutoacha kuibua mambo kama hayo yanayotokea katika vituo  vya kutoa huduma za Afya vya umma na binafsi

Mapema leo kwenye mitandao ya kijamii imesambaa video inayodaiwa kutoka Kivule, Dar es Salaam ya Muhudumu wa Hospitali ya Amana Kivule akisafisha kwa Maji Baridi ya Bomba, Vifaa Vilivyotumika kuhudumia Wagonjwa vikiwemo vya Upasuaji kinyume na taratibu za Kiafya