Friday , 7th Jul , 2023

Watu sita wamefariki dunia na wengine 81 wamepelekwa hospitalini baada ya moto kuzuka katika chumba kimoja katika nyumba ya wastaafu katika mji wa Milan nchini Italia.

Tahadhari  ilitolewa mapema Ijumaa katika nyumba ya Casa dei Coniugi kwa wazee.

Moto huo ulidhibitiwa haraka lakini Meya wa Milan Giuseppe Sala alisema waokoaji walilazimika kumtoa kila mtu "karibu mmoja baada ya mwingine kwa mkono". Meya huyo amewaambia waandishi wa habari kuwa "vifo sita ni idadi kubwa sana".

Hata hivyo, alisema hali inaweza kuwa mbaya zaidi. Ushahidi wote uliashiria moto huo uliotokea katika chumba kimoja ambapo wanawake wawili walikuwa wakiishi.

 Vifo vingine vinne vilisababishwa na kuvuta moshi. Kwa mujibu wa shirika la habari la Ansa, watano kati ya sita waliopoteza maisha  walikuwa wanawake.Mmoja wa wafanyakazi aliibua alitoa taarifa kwa wazima moto . Watu wote waliopelekwa hospitalini walikuwa walidhuriwa  na sumu ya moshi, na 14 wanasemekana kuwa katika hali mbaya.