Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Profesa James Mdoe
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Profesa James Mdoe, wakati akifungua mkutano wa 11 wa wanasayansi katika Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS),amesema elimu ya Tanzania imepiga hatua ikiwemo elimu ya vyuo ambapo kwa chuo cha Muhimbili kimekuwa moja ya vyuo vitano bora barani Afrika hali iliyofanya baadhi ya mataifa kuleta wanafunzi wake kuja kupata elimu.
Kuhusu utafiti Profesa Mdoe amewataka wanasayansi nchini kuendelea kutumia tafiti na kufanya tafiti zitakazoleta tija kwa jamii huku akiahidi serikali kuendelea kusaidia kada ya utafiti nchini kwa kutoa fedha pamoja na kusomesha wanafunzi kwenye kada hiyo.
Kwa upande wake Kaimu Makamu Mkuu wa MUHAS Apolynali Kamambwa, amesema mkutano huo ni sehemu ya mikutano inayofanywa katika chuo hicho ambapo yamesaidia kukifanya chuo hicho kuimarika kielimu na hivyo kuleta matokeo katika kutatua changamoto katika sekta ya afya .