Wednesday , 21st Jun , 2023

Watu watano akiwemo mtoto wa kike mmoja anayekadiriwa kuwa na miaka 8 wamepoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa baada ya gari la New Force linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam kwenda mkoani Rukwa kupata ajali katika Kijiji cha Igando kata ya Luguda Wanging'ombe mkoa wa Njombe.

Basi la New Force lililopata ajali

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe John Makuri Imori, amesema ajali hiyo imetokea leo Juni 21, 2023, majira ya saa 8:30 mchana, baada ya dereva wa basi hilo kutaka kulipita gari lingine bila kuchukua tahadhari na kupoteza mwelekeo na kutumbukia kwenye mtaro.

"Taarifa za awali ni kwamba basi hilo lilikuwa linatoka Dar es Salaam, dereva alitaka ku-overtake lori likapoteza ueleko na kugonga daraja na kuingia mtaraoni, waliofariki mpaka sasa ni wanaume wanne na mtoto mmoja anayekadiriwa kuwa na miaka nane," amesema Kamanda Imori