Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt.Selemani Jafo, akifanya usafi
Ni kauli iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt.Selemani Jafo, mara baada ya kufanya usafi kwenye baadhi ya mitaro ya Jiji la Dodoma na kupanda miti rafiki ya ardhi katika shule ya Sekondari Kiwanja cha Ndege.
Waziri Jafo amesema miradi hiyo yenye lengo la kutunza mazingira katika uendeshwaji wake, imeonesha mafanikiwa ya kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa, huku akitolea mfano wa treni ya mwendokasi, mabasi ya mwendokasi na kutaja athari zilizotokea kabla.
Tanzania inaungana na nchi zingine Duniani kuanza kuadhimisha wiki ya utunzaji Mazingira ambapo imebeba kauli mbiu isemayo "Pinga Uchafuzi wa Mazingira Unaotokana na Taka za Plastiki".